
WhatsApp secured by end-to-end encryption
♤Kwanza si WhatsApp pekee ndio wana hichi kituh tunachokiita end-to-end encryption. Nimechagua tu kuieleza kwa theme ya WhatsApp.
■Kwa ufupi na kwa namna rahisi kabisa end-to-end encryption hii ni namna ya kulinda na kuhakikisha wewe na unaewasiliananae au unaowasiliananao tu, ndio mnaoweza kuona messages《chart》zenu. Pasiwepo na mtu wa kati ataeweza kuona au kuingilia mawasiliano yenu, not even kampuni ya WhatsApp.
☆Message zote zinalindwa. Kila message kila message,picha,voice au video zinalindwa na unique “lock”&”key”. Hivyo wewe na unaemtumia ndio mnaokuana ‘special key & lock’ zinazoitajika kufungua ujumbe wa message uliokua umetumiwa. Na huu ni mchakato hufanyika ‘automatically’ wenyewe hauitaji wewe ufanye setting yoyote.
♡KWA MFANO unarafiki yako anaitwa NGOSWE
Ngoswe anakutumia ujumbe “mambo” huu ujumbe wa Ngoswe kitalaamu tunaita ‘plaintext‘. Sasa hii ni plaintext inakuwa converted kwenda kwenye mfumo ambao hausomeki (unreadable form) kwa kutumia key (mfano key u)
♧So baada ya kuconvert kinachopatiakana hapo tunakiita ciphertext. Mpaka hapo hiyoo ni process tunaiita encryption😎
♢Upande wako sasa, WhatsApp itapokea ciphertext na kui>convert, irudi Kuwa plaintext kwa kutumia key ileile (key u) Hapo sasa ndio utaweza kuisoma, hii nayo ni process kitalaamu huitwa description😆
¤Hivyo na wewe ukituma ujumbe utapitia mtoririko.
●FORMULA encryption & description. Ngoswe (mtumiaji) C=E(mambo, u)
Wewe (mpokeaji) “mambo” D=(C,K)
C>ciphertext,~E>encryption, ~D>description
